UN yafadhaishwa na ongezeko la machafuko Ukingo wa Magharibi
24 Februari 2025Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleezea wasiwasi wake hii leo kufuatia kuongezeka kwa visa vya machafuko vinavyofanywa na walowezi wa Israel kwenye Ukingo wa Magharibi.
Aidha amesema anafadhaishwa na miito ya unyakuzi baada ya Israel kutangaza kupanua operesheni za kijeshi kwenye eneo hilo la Palestina inalolikali kwa mabavu.
Amesema hayo mbele ya Baraza la Haki za Binaadamu la umoja huo mjini Geneva.
Jeshi la Israel lilianza msako mkali dhidi ya wanamgambo wa Kipalestinakaskazini mwa Ukingo wa Magharibi mwezi uliopita, mara baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa katika Ukanda wa Gaza.
Mashambulizi hayo yameongezeka hatua kwa hatua, hadi kwenye kambi nyingi za wakimbizi karibu na miji ya Jenin, Tulkarem na Tubas.