UN yaelezea wasiwasi kuhusu ghasia za Sudan Kusini
25 Aprili 2025Matangazo
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umesema mapigano kati ya jeshi hilo la serikali SSPDF na SPLA-IO katika kaunti jirani za Morobo na Yei kwenye jimboni humo, yamesababisha raia kuhama makazi yao na wengine kujeruhiwa.
Upinzani Sudan kusini wasema uko chini ya mashambulizi mapya
Kamishna wa kaunti ya Morobo Charles Data Bullen, amesema hali katika eneo hilo bado ni tete.
Mgawanyiko waibuka ndani ya chama cha SPLM-IO, Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa haukutoa maelezo zaidi kuhusu mapigano hayo, lakini umehimiza kusitishwa mara moja kwa uhasama hasa kutokana na hali ya kisiasa na kiusalama ambayo tayari ni mbaya .