UhamiajiItaly
Karibu watu 20 wafa maji baada ya boti kuzama
13 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi, UNHCR, nchini Italia, Filippo Ungaro, abiria wengine waliokuwa kwenye boti hiyo iliyokuwa na karibu abiria 100 bado hawajapatikana.
Lakini manusura mmoja amesema boti hiyo ilikuwa na wahamiaji kati ya 92 hadi 97 wakati ilipoondoka Libya. Mamlaka bado zinawatafuta manusura wengine 12 hadi 17, limesema shirika hilo.
Haijajulikana mara moja wahamiaji hao walikaa baharini kwa muda gani.
UNHCR limesema wahamiaji 675 wamekufa wakijaribu kufanya safari hizo hatari za kuvuka Bahari ya Mediterrania kwa mwaka huu tu. Idadi hii haijajumuisha wale waliozama siku za karibuni.