UN: Wasudan Kusini milioni 7.7 wanakabiliwa na "njaa kali"
9 Aprili 2025Eneo la Upper Nile lililo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo limeathiriwa zaidi na mgogoro wa hivi karibuni. Kwa sasa, zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula huku mashirika ya misaada yakihangaika kufikisha msaada kutokana na vurugu.
Tangu ilipopata uhuru wake mwaka 2011, Sudan Kusini, mekuwa ikikaliwa na changamoto ya ukosefu wa usalama na utulivu wa kisiasa. Kwa sasa, migogoro kati ya vikundi vinavyomuunga mkono rais Salva Kiir na makamu wake wa kwanza Riek Machar imezidisha hali kuwa mbaya.
Soma pia: Sudan Kusini yasema Machar aliyekamatwa alijaribu kuchochea uasi
Wakati huo huo shirika la kuwahudumia watoto la UNICEF limeripoti mlipuko wa maradhi ya kipindupindu na kusababisha maambukizi zaidi ya 40,000 na vifo karibu 700, huku watoto wakiwa waathirika wakubwa.
Aidha kupungua kwa misaada ya kimataifa kumewafanya wananchi wa Sudan Kusini kukabiliana na changamoto kubwa zaidi, huku vituo vingi vya afya vijijini vikifungwa.