MigogoroMashariki ya Kati
UN: Wapalestina 1,373 waliuawa wakisubiri misaada huko Gaza
1 Agosti 2025Matangazo
Kati yao, 859 waliuawa karibu na vituo vya shirika la kugawa misaada linaloungwa na Marekani na Israel, la Gaza Humanitarian Foundation, GHF, huku wengine 514 wakipoteza maisha wakiwa njiani kuelekea kwenye misafara ya misaada.
Mnamo Ijumaa pekee, watu 11 wameuawa kutokana na mashambulizi ya anga na risasi za Israel, wakiwemo wawili waliokuwa wakisubiri msaada.
Hayo yamejiri wakati maafisa wawili wa utawala wa Trump – mjumbe maalum Steve Witkoff na balozi wa Marekani nchini Israel Mike Huckabee – wakizuru kituo cha misaada cha GHF huku dunia ikielekeza lawama kwa Israel kutokana na janga la njaa Gaza.