UN: Wanaharakati Kongo wanakabiliwa na hatari kubwa
5 Machi 2025Matangazo
Hayo yameelezwa leo na Mtaalam wa Umoja wa Mataifa Mary Lawlor ambaye ameelezea wasiwasi wake juu ya hali hiyo na kutoa wito wa kupatikana msaada utakaowezesha zoezi la kuwahamishwa kwa wanaharakati hao.
Mtaalamu huyo ameongeza kuwa wanaharakati hao wanaishi kwa hofu huku akieleza kuwa waasi wa M23 wanaorodhesha majina ya wanaharakati watakaokamatwa katika maeneo yakioko chini ya udhibiti wao.
UNHCR: Watu 800,000 waikimbia Kongo kutokana na mzozo
Haya yanajiri wakati shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR limesema kuwa takriban watu 80,000 wanaokimbia vita vya mashariki mwa Kongo wamepata hifadhi katika nchi jirani, huku Burundi ikipokea idadi kubwa ya wakimbizi hao.