Wafanyakazi 383 wa misaada wauawa kwenye maeneo ya vita 2024
19 Agosti 2025Matangazo
Kulingana na OCHA, nusu ya idadi hiyo waliuawa Gaza wakati wa vita kati ya Israel na Hamas.
Mratibu Mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher amesema idadi hiyo ya mauaji inapaswa kuwa tahadhari ya kuwalinda raia wanaokwama kwenye maeneo ya mizozo na wote wanaojaribu kuwasaidia.
Katika taarifa yake ya kuangazia Siku ya Misaada ya Kiutu Duniani inayoadhimishwa kila Agosti 19, Fletcher amesema mashambulizi katika kiwango hicho cha jumuia ya kimataifa kutowajibika na kuchukua hatua, yanatia aibu.
Kanzidata ya usalama wa wafanyakazi wa kutoa misaada, ambayo imekusanya ripoti tangu mwaka 1997, imeonyesha kuwa mauaji yaliongezeka kutoka 293 mwaka 2023 hadi 383 mwaka 2024, ikiwemo zaidi ya 180 katika Ukanda wa Gaza.