UN: Vyombo vya habari vinalengwa na magenge ya wahalifu
21 Machi 2025Umoja wa Mataifa pia umesifu ujasiri wa waandishi wa habari wanaofanya kazi katika nchi ya Carribean katika mazingira magumu.
Eric Voli Bi, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) huko nchini Haiti, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hali inatisha na kutia wasiwasi kwa sababu vyombo vya habari vimekuwa vikilengwa na kuteketezwa.
Soma pia: Marekani yasitisha mchango kwa kikosi cha amani Haiti
Desemba mwaka jana, waandishi wawili wa habari waliuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince walipokuwa wakiripoti kuhusu kufunguliwa tena kwa hospitali.
Wiki iliyopita, ofisi za kituo cha televisheni na vituo viwili vya redio vilishambuliwa na kuporwa, huku jiji hilo likikabiliwa na wimbi jipya la ghasia za magenge ya wahalifu.