MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
UN: Vita vya DRC vyapelekea watu 100,000 kuwa wakimbizi
22 Machi 2025Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi kubwa ya watu hao wanaishi katika mazingira duni kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wake.
Mapigano makali yalizuka eneo hilo katika miezi ya hivi karibuni kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, vita vinavyoendelea kusababisha maafa makubwa na vikitishia kusababisha mzozo mpana zaidi wa kikanda.