UN: Vita vya Iran na Israel vyachochea mzozo wa wakimbizi
21 Juni 2025Matangazo
UNHCR imeyahimiza mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, kuheshimu haki za watu kutafuta usalama sehemu walizochagua na kuwezesha hilo chini ya kanuni za kibinadamu.
Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi, amesema ukanda huo tayari umekumbwa na vita, hasara, na kuhamishwa kwa idadi kubwa ya watu na kwamba hawawezi kuruhusu madhila mengine ya wakimbizi kukita mizizi.
Maelfu ya Wairan waandamana kuipinga Israel
Grandi pia amesema, ni wakati sasa wa kutuliza hali hiyo kwa kuwa mara tu watu wanapolazimishwa kukimbia, hakuna njia ya haraka ya wao kurejea makwao na mara nyingi matokeo yake huwa ya kudumu na hushuhudiwa vizazi na vizazi.