UchumiAngola
UN: Uchunguzi ufanyike kuhusu maandamano nchini Angola
1 Agosti 2025Matangazo
Msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amesema mbali na vifo hivyo, watu wengine karibu 1,000 wanashikiliwa na polisi, huku akiongeza kuwa picha ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa vikosi vya usalama vya Angola vilitumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji, jambo ambalo linaashiria matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima wala uwiano."
Ghasia zilizuka siku ya Jumatatu kufuatia mgomo ulioitishwa na madereva teksi waliopinga ongezeko la bei ya mafuta. Hayo yalikuwa ni machafuko mabaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye utajiri mkubwa wa mafuta ambapo mamilioni ya watu wanaishi katika umaskini.