UN: Taliban inatekeleza ukiukwaji wa haki za binaadamu
24 Julai 2025Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo imedokeza kwamba walio katika hatari kubwa ya kulipizwa kisasi na kufanyiwa ukiukaji mwingine wa haki za binadamu ni wanawake na wasichana, pamoja na watu waliokuwa wakifanya kazi na serikali ya zamani na vikosi vyake vya usalama na wanahabari.
Ripoti hiyo iliyotolewa kwa pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imetokana na mahojiano na Waafghani 49 waliorejea nchini.
Hata hivyo serikali ya Taliban imewahi kukanusha madai ya unyanyasaji, ikisema kuwa imetangaza msamaha kwa wale wote waliokuwa wakifanya kazi na vikosi vya Jumuiya ya kujihami ya NATO na serikali ya zamani wakati wa vita vyao vya miongo miwili dhidi ya waasi wa Taliban.