MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
UN: Raia 169 waliuawa na M23 mwezi Julai mashariki mwa DRC
31 Julai 2025Matangazo
Kulingana na taarifa za Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Haki za Kibinadamu huko Kongo (UNJHRO), operesheni ya M23 iliyopelekea mauaji hayo ilianza Julai 9 katika eneo la Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Kiongozi wa M23 Bertrand Bisimwa ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa watafanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hiyo lakini akasema kuwa ripoti hiyo inaweza kuwa "kampeni ya udanganyifu".
Hayo yanajiri wakati utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump ukisimamia juhudi za amani kati ya Kongo na Rwanda kwa lengo la kuwezesha miradi ya uwekezaji wa mabilioni ya dola kwenye suala zima la madini.