MigogoroSudan Kusini
Mapigano Sudan yasababisha watu 50,000 kuyakimbia makazi yao
18 Machi 2025Matangazo
Haya yamesemwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.
Mratibu wa Misaada ya Kibinaadamu nchini Sudan Kusini Anita Kiki Gbeho, amesema nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya kutumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Soma pia: Sudan yaishtaki UAE kwenye mahakama ya ICJ
Katika taarifa yake, Gbeho, amesema vurugu hizo zinaziweka jamii hatarini na kulazimisha kusimamishwa kwa huduma za kuokoa maisha.
OCHA imesema watu 10,000 kati ya waliokimbia makazi yao wamevuka mpaka na kuingia Ethiopia.
Shirika hilo limeongeza kusema kuwa wafanyakazi 23 wa mashirika ya misaada pia wamelazimika kuondoka katika eneo hilo, huku kituo cha kuwatibu wagonjwa wa kipindupindu kikifungwa katika eneo la Nasir.