UN: Magenge Haiti kuchukua udhibiti kamili wa mji mkuu
3 Julai 2025Umoja wa Mataifa umeongeza kwamba mamlaka za nchi hiyo ya Carribean zimeshindwa kukomesha vurugu zinazoongezeka.
Afisa wa Umoja huo Ghada Fathy Waly ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba inakadiriwa asilimia 90 ya mji mkuu huo sasa unadhibitiwa na makundi ya wahalifu ambayo yametanua mashambulizi yao.
Magenge ya wahalifu ya Haiti yanatumia ombwe la utawala na uhaba wa huduma za umma ili kuanzisha utawala pinzani. Magenge hayo yamekuwa yakizuia barabara kuu na hivyo kuvuruga shughuli za biashara na kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa muhimu ikiwemo chakula.
Ujumbe wa kulinda amani unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ukiongozwa na polisi wa Kenya uliwasili Haiti mwaka jana ili kusaidia kukomesha ghasia za magenge hayo, lakini unakabiliwa na uhaba wa askari, vifaa na ufadhili mdogo.