MigogoroIran
UN kujadili hifadhi inayoongezeka ya urani nchini Iran
11 Machi 2025Matangazo
Wanadiplomasia wamesema jana Jumatatu kwamba kikao hicho kinafuatia ombi la mataifa sita kati ya 15 wanachama, ambayo ni Ufaransa, Ugiriki, Panama, Korea Kusini, Uingereza na Marekani.
Mataifa hayo aidha yanalitaka baraza hilo kujadili wajibu wa Iran wa kulipatia Shirika la Umoja huo la nguvu za Atomiki, IAEA taarifa muhimu za kuthibitisha masuala kadhaa yanayohusiana na maeneo mbalimbali ya nyuklia yaliyogunduliwa, lakini hayakutangazwa.
Iran inakana madai kwamba inanuia kutengeneza silaha ya nyuklia ingawa imeongeza kasi ya urutubishaji wa madini ya urani hadi asilimia 60 na kukaribia asilimia 90 ambayo ni kiwango cha kutengeneza silaha.