MigogoroAfrika
UN ina wasiwasi na hatua ya kusonga mbele ya M23
21 Februari 2025Matangazo
Umoja wa Mataifa umetowa tahadhari hiyo jana Jumatano, ukionesha msisitizo wa kitisho cha uwezekano wa mgogoro huo kuwa wa kikanda.
Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja huo wa Mataifa katika eneo la maziwa makuu, Huang Xia, amesema ikiwa taarifa walizo nazo ni sahihi, basi inaonesha kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda linaendelea kusonga mbele kuelekea maeneo muhimu ya kimkakati katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini.
Soma pia:UN ina wasiwasi na hatua ya kusonga mbele ya M23
Wakati huo huo, mkuu wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja huo nchini Kongo Bintou Keita, pia amezungumzia wasiwasi wake kuhusu kusonga mbele kwa M23 ambao hivi sasa wako katika eneo la makutano ya mipaka kati ya Kongo, Rwanda na Burundi.