UN: Haki za wanawake ziliendelea kukandamizwa ulimwenguni
6 Machi 2025Matangazo
Ripoti hiyo inasema ukandamizaji huo umetokana na sababu mbalimbali zikiwemo zinazohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi hadi kurudi nyuma kwa demokrasia.
Ripoti hiyo inaonesha kwamba kudhoofika kwa taasisi za kidemokrasia katika mataifa yaliyotajwa, kumekwenda sambamba na kukandamizwa kwa usawa wa kijinsia.
Umoja wa Mataifa umegusia pia kuhusu kuongezeka maradufu kwa uwakilishaji wa wanawake kwenye mabunge duniani tangu mwaka 1995, lakini bado wanaume ndio wanaohodhi kiasi robo tatu ya mabunge duniani.