UN: Gaza ni “makaburi” huku sheria za kimataifa zikidhoofika
8 Septemba 2025Akizungumza mjini Geneva wakati wa kikao cha 60 cha Baraza la Haki za Binadamu,Turk alishutumu mauaji ya maelfu ya raia wa Kipalestina, mateso yasiyoelezeka na uharibifu mkubwa wa makazi na miundombinu.
Alisema: "Israel's mass killing of Palestinian civilians in Gaza; its hindering of lifesaving aid na njaa inayosababishwa; mauaji ya waandishi wa habari na uhalifu wa kivita mara kwa mara—vyote hivi vinaishtua dhamiri ya dunia.”
Turk aliongeza kuwa Israel ina "kesi ya kujibu ICJ” kufuatia uamuzi wa Januari kwamba taifa hilo lina wajibu wa kisheria kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari na kuhakikisha misaada inawafikia Wapalestina.
Gaza ni "makaburi”
"Gaza is a graveyard,” alisema, akisisitiza kuwa eneo hilo "linalia kwa ajili ya amani.” Pia alikumbusha kwamba Israel bado iko kwenye majeraha makubwa baada ya shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023, lililoua watu 1,200 na kupelekea kutekwa kwa mateka 251.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, kampeni ya kijeshi ya Israel imeua karibu watu 63,000. Wakati huo huo, wachunguzi wa njaa duniani wanasema sehemu ya eneo la Gaza tayari imeingia kwenye njaa.
Msimamo wa Israel
Ujumbe wa Israel katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva umesema utajibu maombi ya maoni hivi karibuni. Nchi hiyo mara kwa mara imekanusha madai ya mauaji ya kimbari, ikisisitiza haki yake ya kujilinda dhidi ya Hamas.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ameapa kuendeleza operesheni za kijeshi Gaza City, licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa karibu watu milioni moja bado wamekwama katika eneo hilo na hali ya njaa kutangazwa rasmi mwezi uliopita.
Sheria za kimataifa zikidhoofika
Turk hakulenga Gaza pekee. Alisema misingi ya sheria za kimataifa na haki za binadamu duniani inadhoofishwa na "mitindo ya kutisha” ikiwemo propaganda za vita na baadhi ya mataifa kujiondoa kwenye mfumo wa pande nyingi.
"Sheria za vita zinachanwa vipande vipande – bila kuwapo uwajibikaji wowote wa maana,” alisema, akitaja uvunjaji mkubwa wa sheria za kimataifa nchini Ukraine, Sudan, Myanmar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aidha, alionya dhidi ya kuabudu vita, akitaja gwaride kubwa la kijeshi lililoandaliwa na China na hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kubadilisha jina la Wizara ya Ulinzi kuwa Wizara ya Vita. "Hakuna gwaride la amani, wala wizara za amani,” alisema.
Wito wa kuchukua hatua sasa
Kwa maneno yake ya mwisho, Turk alisema jumuiya ya kimataifa "inashindwa kuwasaidia watu wa Gaza.” Alitoa wito wa kuchukua hatua sasa ili "kukomesha umwagaji damu huu” na kuzuia dunia kuangukia tena katika historia ya giza, akitaja Holocaust na Vita Kuu Mbili kama mifano ya onyo.
Chanzo: AFPE,RTRE