Umoja wa Ulaya wamrai Rais Kiir kumwachia Machar
28 Machi 2025Matangazo
Hatua hiyo inafuatia kukamatwa kwa Riek Machar huku hofu ikiongezeka kuwa nchi hiyo ipo kwenye hatari ya kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Umoja wa Ulaya umesema kukamatwa kwa Machar siku ya Jumatano kunaashiria kuongezeka kwa hali ya wasiwasi ambayo imekuwepo kwa siku za karibuni katika nchi hiyo changa zaidi duniani.
Zaidi ya washirika 20 wa Machar wa kisiasa na kijeshi katika serikali ya umoja wa kitaifa wamekamatwa tangu mwezi Februari, na wengi wao wakiwa wamezuiliwa.
Itakumbukwa kuwa kati ya mwaka 2013 hadi 2018 nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na watu takriban watu 400,000 walipoteza maisha.