Umoja wa Ulaya kuiondolea Syria vikwazo vya kiuchumi
20 Mei 2025Matangazo
Wanadiplomasia kutoka nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano ya awali ya hatua hiyo, ambayo inapaswa kutangazwa rasmi baadae Jumanne na mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo wanaokutana Brussels, Ubelgiji.
Uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya umechukuliwa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump wiki iliyopita, kutangaza kuiondolea vikwazo Syria.
Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamesema makubaliano hayo yanapaswa kuhakikisha vikwazo vya kuzifungia benki za Syria kujihusisha na mfumo wa kimataifa na kuzuia mali za benki kuu vinaondolewa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Asaad al-Shaibani, amesema hatua hiyo inaonyesha ''nia ya kimataifa'' ya kuiunga mkono Syria.