Umoja wa Ulaya wakosoa nyongeza ya ushuru ya Trump
31 Mei 2025Matangazo
Msemaji wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya amesema kanda hiyo imefadhaishwa na uamuzi wa Marekani wa kupandisha ushuru wa chuma kinachoagizwa njea kutoka asilimia 25 hadi 50.
Afisa huyo amesema hatua hiyo inaongeza mashaka kwenye uchumi wa dunia na kupandisha gharama kwa biashara na wanunuzi wa pande zote mbili. Umoja huo wenyewe umeahidi kutangaza hatua za kujibu mapigo kabla ya kuanza majira ya kiangazi.
Rais Trump alitoa tangazo hilo jana Ijumaa akiahidi kwamba kiwango hicho kikubwa cha ushuru kitaimarisha sekta ya ufuaji chuma nchini Marekani.