EU yaanza kusitisha vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea Syria
24 Februari 2025Matangazo
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wameamua hii leo kuanza kusitisha vikwazo dhidi ya Syria baada ya kuanguka kwa utawala wa muda mrefu wa Bashar al-Assad.
Taarifa kwa waandishi wa habari imesema Ulaya itandoa vikwazo kwenye sekta za nishati, usafirishaji na benki ili kulisaidia taifa hilo kuimarisha uchumi wake kwa haraka, kujijenga upya na kurejesha utulivu.
Taasisi za kifedha za Ulaya sasa zitaruhusiwa kuendeleza ushirikiano na Benki za Syria chini ya masharti fulani yatakayowezesha miamala kwa ajili ya ujenzi.Viongozi wa EU watahadharisha kuhusu mustakabali wa Syria
Uamuzi huo unaanza kutekelezwa kesho Jumanne baada ya kuchapishwa kwenye Jarida Rasmi la Umoja wa Ulaya.