Umoja wa Ulaya uko tayari kwa mazungumzo magumu na Marekani
4 Februari 2025Matangazo
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesema umoja huo utashughulikia mambo kwa uhalisia katika kujaribu kupata suluhu, wakati ikijiandaa na tangazo la Rais Donald Trump wa Marekani la kuzitoza ushuru bidhaa za umoja huo.
''Tutakuwa tayari kwa mazungumzo magumu inapohitajika, na kutafuta suluhu inapowezekana, kutatua malalamiko yoyote na kuweka misingi ya ushirikiano imara,'' alisema Ursula von der Leyen.
Ulaya yaapa kujibu mapigo iwapo Marekani itaongeza ushuru
Akizungumza mapema mjini Brussels kwenye mkutano na mabalozi wa Ulaya, Von der Leyen amesema kuna mengi ambayo yako hatarini kwa pande zote, lakini ameahidi kusimama imara wakati Ulaya itakapokuwa inakabiliana na Marekani.