Ulaya yakhofia athari za ushuru kwa dunia
7 Aprili 2025
Marekani ilitangaza mwezi Machi, ushuru wa asilimia hadi 25 kwa bidhaa za chuma na aluminium kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na washirika wake wengine wa kibiashara.
Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen amesema Umoja wa Ulaya unatoa fursa kwa Marekani kufikia makubaliano ya pande zote kuondoa ushuru wote dhidi ya bidhaa za viwandani. Soma pia: Trump atangaza ushuru mpya wa magari yanayoagizwa kutoka nje
Kiongozi huyo wa juu katika Umoja wa Ulaya, ametoa mwelekeo huo baada ya kuzungumza na wakuu wa viwanda vya chuma na bati katika wakati ambapo, bidhaa za kutoka nchi za Umoja huo zikikabiliwa na kitisho cha kutozwa ushuru wa asilimia 20 kuanzia Jumatano.Soma pia:Ushuru uliotangazwa na Trump waanza kutekelezwa
Mkuu wa masuala ya biashara katika Umoja huo Maros Sefcovic amesema taasisi hiyo itatumia njia zote kujilinda dhidi ya athari za ushuru wa rais Trump.