EU kuweka vikwazo kuhusu uvamizi wa M23 Congo
15 Machi 2025Matangazo
Umoja wa Ulaya unajiandaa kuwawekea vikwazo watu kiasi kumi kuhusu operesheni ya waasi wa kundi la M3 wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hayo yamesemwa jana Ijumaa na wanadiplomasia, ingawa hawakufafanua ikiwa vikwazo hivyo vitawajumuisha maafisa wa Rwanda wanaotuhumiwa kuchochea mapigano.
Vikwazo hivyo vinatarajiwa kutangazwa rasmi katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika Jumatatu ijayo mjini Brussels.