Umoja wa Ulaya kurejesha upya vikwazo dhidi ya Urusi
28 Januari 2025Uamuzi huu ulifikiwa baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa Umoja huo siku ya Jumatatu, ambapo viongozi hao walitowa wito wa kuwa na msimamo wa pamoja katika kufanya kazi na Rais Donald Trump wa Marekani kutokana na kile wachambuzi wanachokiita sera ya gawa uwatawale.
, alisema wakati Marekani ikitekeleza sera ya nje inayojikita kwenye kuuza na kununuwa, Ulaya inahitaji kujiweka pamoja, kwani umoja ni nguvu.
Afisa wa programu katika Mfuko wa Marshall wa Ujerumani, Zsuzsanna Vegh, alisema Trump anadhamiria kuudhoofisha Umoja wa Ulaya na badala yake awe anafanya kazi na nchi moja moja.
Soma pia:Trump ausuta Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Davos
Akizungumza na DW, afisa huyo alisema "Viongozi wa Ulaya wakishindana kupata kuonekana na utawala wa Trump kutakuwa na athari mbaya kwa umoja ndani ya Muungano wa Ulaya. Na uungaji mkono wa Trump kwa makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia barani Ulaya unaweza kuudhoofisha Muungano huo."
Ambapo hakuna anayejuwa vipi hasa sera za Trump zitakavyokuwa ndani ya wiki zijazo, na khofu ya vita vya kibiashara inaendelea kuwa kubwa, kuna matumaini kwamba anaweza asiwe mwepesi mbele ya Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Chini kwa chini, wanadiplomasia wa Ulaya wanaonekana kufurahika kwamba Trump ameitishia Urusi kuiwekea ushuru wa hali ya juu na hata vikwazo zaidi endapo haitakomesha vita vyake dhidi ya Ukraine.
Kallas alisema ni jambo zuri kwamba Trump aliweka mbinyo zaidi kwa Urusi na kuiambia wazi kwamba suala la kuvimaliza vita vya Ukraine liko mikononi mwa Putin.
Matamshi ya Trump dhidi ya Urusi
Watu wa Ulaya wanayachukulia maneno makali ya Trump dhidi ya Urusi kama ishara njema. Wataalamu wanasema msimamo wa rais huyo wa Marekani ulimpa mshangao mkubwa zaidi Waziri Mkuu Viktor Orban wa Hungary, sahibu mkubwa wa Putin, kuliko viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya.
Umoja wa UIaya ulirejesha upya vikwazo vyake vya biashara dhidi ya Urusi na kuzuwia mali zenye thamani ya mabilioni ya euro.
Kupitia mtandao wa X, Kallas aliandika kwamba Umoja huo umetekeleza ahadi yake, na kwamba vikwazo hivyo vitaendelea kuinyima Moscow fedha za kuendeshea vita vyake, kwani Urusi inalazimika kulipia gharama kwa madhara inayoyasababisha.
Orban amekuwa akikwamisha mchakato huu na aliwahi kutishia kupigia kura hatua yoyote ya kuongeza muda wa vikwazo hivyo ikiwa Umoja wa Ulaya haukuilazimisha Ukraine kusafirisha gesi ya Urusi kupitia mabomba yake kuelekea Hungary.
Soma pia:Urusi yaishambulia Ukraine, kusabisha kifo cha mtu mmoja
Mapema mwezi huu, Ukraine iliamua kutokuongeza muda wa makubaliano ya kuiruhusu gesi ya Urusi kupitia kwenye nchi yake.
Orban alisema anazuwia kuongezwa kwa vikwazo na alidai nchi yake ilikuwa inapoteza mabilioni tangu Ukraine izuwie usambazaji wa gesi ya Urusi.Umoja wa Ulaya wasema uko tayari kuzungumza na Marekani kurekebisha mahusiano na China
"Ikiwa Ukraine inataka msaada kuwawekea vikwazo Warusi, watakeni wafunguwe bomba la gesi na waziruhusu nchi za Ulaya ya Kati, ikiwemo Hungary, kuingiza gesi hiyo kupitia Ukraine." Alisema Waziri Mkuu huyo wa Hungary.
Lakini baadaye, Orban aliachana na madai yake hayo na kusalimu amri mbele ya matakwa ya Umoja wa Ulaya kuiadabisha Urusi.
Kilichomfanya abwage manyanga, ni ahadi ya Kamisheni ya Ulaya kwamba ingeliendelea na majadiliano na Ukraine juu ya usambazaji wa gesi barani Ulaya kupitia mfumo wa mabomba ya nchi hiyo na kwa mujibu wa wajibu wa kimataifa ilionao Ukraine.
Kamisheni hiyo pia ilisema itazishirikisha Hungary na Slovakia kwenye mchakato huo.
Lakini Kamisheni hiyo haikusema chochote endapo itaiomba Ukraine kurudi kwenye mkataba wa kusambaza gesi ya Urusi kupitia mabomba yake, huku Rais Volodymyr Zelensky akisema wazi kwamba kamwe "Ukraine haitawaicha Urusi ifaidike kupitia ardhi yake."