Umoja wa Ulaya kupendekeza kanuni kali kuwaondoa wahamiaji
11 Machi 2025Mswada huo mpya unalenga kuwezesha mchakato wa ufanisi zaidi pamoja na kuongeza idadi ya kukata maombi ya hifadhi.
Kulingana na halmashauri hiyo, kwa sasa, karibu moja ya tano ya watu wanaoamriwa kuondoka katika nchi za Umoja huo, kweli hurudi katika nchi zao za asili.
Waomba hifadhi wengi waliokataliwa husalia katika nchi walizokataliwa, licha ya uamuzi dhidi yao kwa sababu nchi zao za asili hukataa kuwakubali ama taratibu huchukua muda mrefu zaidi kutekelezwa.
Chini ya pendekezo hilo, maamuzi ya kurejeshwa makwao kwa waomba hifadhi yatakayofanywa na nchi moja ya Umoja wa Ulaya yatatumika na nchi nyingine wanachama.
Kamishna wa uhamiaji wa Umoja huo, Magnus Brunner, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba haikubaliki kwa utaratibu wa kutoa hifadhi kukamilishwa katika moja ya nchi mwanachama na kisha utaratibu mwingine kuanzishwa katika nchi nyingine.