Umoja wa Ulaya kujifunza kutokana na kupotea umeme Iberia
29 Aprili 2025Matangazo
Msemaji mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya Paula Pinho amesema kwa kushirikiana kwa karibu na waendeshaji na wasimamizi wa gridi ya taifa ya umeme, makao makuu ya umoja wa Ulaya mjini Brussels yatachunguza kwa makini sababu zilizopelekea umeme kupotea Uhispania na Ureno, kwa umbali gani Umoja wa Ulaya umejiandaa vyema na ni masomo gani yanayoweza kupatikana kutoka kwa tukio kama hilo.
Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema serikali yake imeanzisha tume maalumu kuchunguza sababu za kupotea kwa umeme nchi nzima.
Akizungumza na vyombo vya habari siku moja baada ya Uhispania na Ureno kukabiliwa na giza kwa sababu ambazo hazijajulikana, waziri mkuu Pedro pia amesema hatua zote zitachukuliwa kuhakikisha umeme haupotei tena.