Umoja wa Ulaya kuendeleza vikwazo dhidi ya Urusi
27 Januari 2025Matangazo
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema anatarajia uamuzi wa kuendelezwa vikwazo hivyo utafikiwa, licha ya Hungary kusema mapema mwezi huu kuwa bado haijaamua iwapo itaunga mkono hatua hiyo.
Uamuzi kama huo unatakiwa kuungwa mkono na wanachama wote kabla ya kuidhinishwa rasmi. Duru mbalimbali za wanadiplomasia wa Ulaya zimeeleza kuwa makubaliano yamefikiwa na waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ambayo yataifanya nchi hiyo kuafiki mpango huo.
Soma pia:Ujerumani yaijaribu EU kwa kuongeza udhibiti mipakani
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amethibitisha kuwa vikwazo hivyo dhidi ya Urusi vitaendelezwa.