Umoja wa Ulaya: Hakuna mbadala wa diplomasia kuhusu Iran.
11 Aprili 2025Matangazo
Umoja wa Ulaya unasema hakuna mbadala wa diplomasia katika kuutanzua mkwamo kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran kabla kufanyika mazungumzo kati ya Iran na Marekani kesho Jumamosi mjini Muscat nchini Oman.
Msemaji wa afisi inayoshughulikia sera ya kigeni ya Umoja wa Ulaya, Anouar El Anouni amesema umoja huo unatambua juu ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran na kwamba maendeleo yoyote yanayoongeza fursa za kupatikana suluhisho la kidplomasia ni hatua inayoelekea katika mkondo sahihi.
Mazungumzo ya kesho yanalenga kufikia mkataba wa nyuklia huku Iran ikisema inataka mkataba wa haki na Marekani.